Msanii: Willy Paul | Download Nyimbo Mpya za Sauti na Video pamoja Na Maelezo Mafupi

Willy Paul

Acha tuongee ukweli, Willy Paul ni yule mzee wa “love him or hate him”—hawezi pita kimya kama uko kwenye vichochoro vya muziki wa Kenya. Huwezi sema hujamwona; ata kama ulikuwa unajaribu ku-ignore, bado nyimbo zake zinakupata tu.

Jina lake kamili? Wilson Abubakar Radido. Lakini nani anatumia? Ni Willy Paul kila mahali. Jamaa alizaliwa Mathare, ile place watu wanatoka na story za struggle—hapa hakuna shortcuts wala silver spoon. Fikiria baba yake alikuwa seremala anachapa kazi mtaani, na mama anafanyia saloon ili familia ipate ugali. Hapo hakuna cha kulalia laurels, ni hustle from day one.

Shule ikaingia na ika-exit haraka—2011 ameshachapa mwendo. Pesa zilikuwa scarce, bro. Sasa mambo yalipoanza kubadilika, ni pale alipodondosha “Rabuka”—lakini “Sitolia” ndo ilimtoa kabisa, especially akiwa na Gloria Muliro. Lakini, si ati ilikuwa smooth. Jamaa na Gloria wakaingia bifu – beef ya injili, imagine. Willy anasema amebanwa kimasilahi, Gloria naye anajitetea. Drama ilishika headlines. Baada ya kelele, wakaimba “Kitanzi” pamoja, na hiyo ngoma pia iliwasha moto. Kama hujaiskia, honestly, uko chini ya jiwe gani?

2012 inaingia, jamaa anaonekana Kisima Music Awards courtesy ya manager wake, David Grey. Miaka ilisonga hadi 2013, ambapo tuzo za Groove zilitolewa—Willy M. aliibuka Mwanamume Bora, huku Gloria Muliro akiwa Mwanamke Bora. Watu wa gospel walikuwa on fire hiyo time, usicheze.

Na si ati Willy Paul ni lone ranger. Huyu jamaa anapenda collabo kama vile watu wanapenda chai asubuhi. Weka pamoja Alaine wa Jamaica (“I Do”), Nandy wa Bongo (“Njiwa,” “Hallelujah”), Rayvanny (“Mmmh”), Yemi Alade (“Nobody”), mpaka Cecil (“Sikireti”). Huyu mzee anakusanya international features kama vile watu wanavyokusanya likes Instagram. Halafu banger zake za solo? “Jigi Jigi,” “Kanungo,” “Malingo,” na of course “You Never Know”—hiyo ilimpeleka States, bro! Kutoka Mathare hadi Marekani, hiyo ni safari.

Lakini msidhanie anaishi kwa beat tu. Willy ni CEO wa Saldido International Entertainment. Jamaa anabalance biashara na artistry bila stress. Lazima umpe props, ama?

Nyimbp Mpya kabisa za Willy Paul

TOPWAP.LT