Masharti

SoundFlava – Vigezo na Masharti.

Karibu SoundFlava – hapa ndiyo stesheni kuu la mziki wa Afrika Mashariki! Kabla hujaanza kula bata na ngoma zetu, kuna mambo machache ya msingi. Unatumia tovuti yetu [https://soundflava.com/sw] na huduma zetu? Basi, ni lazima ukubaliane na haya masharti – hakuna kubahatisha hapa.

Akaunti Yako: Bro, dada, ni jukumu lako kulinda akaunti yako. Usiache password iko wazi kama mlango wa bucha.

Matumizi: Tumia huduma zetu vizuri. Hakuna ujanja ujanja au matusi. Heshimiana!

Haki Miliki: Hii ni kubwa. Usilete nyimbo au maudhui ambayo si yako. Usivunje hakimiliki za mtu, tutakuchomea cheti.

Leseni ya Maudhui: Ukipakia content hapa, unaturuhusu tuiweke hewani, tuisambaze, tufanye mambo yetu – lakini bado ni yako.

Umiliki: SoundFlava inamiliki vitu vyote vya kwenye site, lakini kile ulichopakia ni mali yako.

Huduma Zetu: Tunakupa huduma “kama ilivyo.” Usije ukalalamika, “mbona audio haifunguki?” – mambo kama hayo hutokea. Hakuna warranty hapa.

Viungo na Dhima: Tukikupeleka kwenye site ya mtu mwingine na mambo yaharibike, hiyo sio yetu. Pia, hatutoi fidia juu ya madhara yasiyo ya moja kwa moja.

Kikomo: Kama kuna shida, kiwango cha dhima ni kile ulicholipa mwaka uliopita – kama ulilipa.

Kulinda SoundFlava: Ukifanya madhambi, wewe ndiye utatetea SoundFlava kwenye kesi. Usituletee balaa.

Sheria: Tunafuata sheria za Tanzania. Ukiwa na shida, tutaleta hoja mahakamani hapa hapa nchini.

Marekebisho: Tunaweza kubadilisha masharti haya muda wowote. Ukiendelea kutumia huduma, unakubali mabadiliko. So, pitia mara kwa mara.

Maswali? Usijisikie vibaya – tuma email: [email protected]

Ahsante kwa kuskiza na kufurahia SoundFlava – hapa ni ngoma tu na vibe kali!


TOPWAP.LT