Msanii: Msaga Sumu | Download Nyimbo Mpya za Sauti na Video pamoja Na Maelezo Mafupi

Jamaa huyu, jina halisi Selemani Jabir Msonjele, lakini ukiita Msaga Sumu ndo wengi wanamjua—mtoto wa Dar es Salaam, the city that never sleeps aisee.
Msaga Sumu siyo jina la mzaha kwenye game ya Singeli. Ni mwandishi, ni performer, ni staa wa mtaa. Akijibebea Kandoro Baba Entertainment mgongoni, msanii huyu amefanya Singeli iwe balaa kwenye mitandao za kijamii—streams kibao, downloads za kutosha, na watu wakimsifia kila kona. Ile ngoma yake “Achi Menengule?” Usiulize, ilichafua Kenya, hadi watu hawataki kuisikia ikiisha. Ilikuwa kama wimbo wa taifa kwao for a minute.
Msaga Sumu si juzi tu ameanza—ana miaka kama 15 akichana kwenye Singeli, akichochea mpaka watu wameanza ku-copy staili zake. Muziki wenyewe, Singeli, ni ule wa kasi, beats kali, lyrics zinatoka kama risasi. Msaga Sumu alianza kupiga shows live back in 2007, halafu 2012 akaingia studio kurekodi rasmi. Kwa kutoa Album yake ya Mwanaume Mashine Mwaka 2018 , watu wakamtambua kama msanii wa kwanza kutoa full Album ya Singeli na hapo ndio Mafanikio yake yaliazia.
Ukichora list ya ngoma zake zinazobamba, usijidanganye ukakosa “Mama wa Kambo,” “Babu wa Luanga,” “Uswahilini Sihami,” “Unanitega Shemeji,” na “Mwanaume Mashine.”
Msaga Sumu: hajategemea kiki pekee bali amejitolea kuwajengea uwezo vijana wa mitaani kupitia kituo chake cha Uswazi Born Talented (UBT). Hapa ndo wanapata mentorship, wanakua wasanii, na yeye mwenyewe anaitwa “Mfalme wa Uswahilini”—hii ni heshima ya mtaa, bro.
Kwa sasa, Msaga Sumu anavunja mipaka ya Singeli, anafanya genre hii ipate heshima Tanzania nzima na nje pia. Hadi hivi sasa, Muziki wa Singeli umeweza kutambuliwa rasmi na serikali kwamba ni moja ya utambulisho wa muziki wetu wa Tanzania. Msaga Sumu? Bila yeye, huwezi taja Singeli ukajisikia salama.