Msanii: Harmonize | Download Nyimbo Mpya za Sauti na Video pamoja Na Maelezo Mafupi

Harmonize

Sasa, Harmonize—yule jamaa wa Bongo aliyekuja juu kama roketi mwishoni mwa 2010s—si tu msanii wa kawaida. Jamaa anaimba, anaandika ngoma, anacheza, basically, anakamua kila kona ya game. Alichanganya Bongo Fleva na Afro-pop ukapata ile vibe ya kipekee, ile inakufanya usimame kwenye dancefloor bila hata kujua. “Kwa Ngwaru” na Diamond Platnumz? Hiyo ilikuwa banger, bro. Na ile albamu yake ya 2020, Afro East, aliwashirikisha kina Yemi Alade na Morgan Heritage—hapo ndo alionyesha hana mipaka.

Lakini usisahau, kabla ya haya yote, alikuwa anaitwa Rajabu Abdul Kahali—au ukitaka Konde Boy. Alianza kujulikana 2015 na “Aiyola,” ngoma laini yenye melody kali. Mwaka uliofuata kidogo, akatupia ngoma “Bado”—ile tu ikamtoa kimasomaso, akashinda ile tuzo ya WatsUp Africa Music Video Award kama Msanii Chipukizi Bora wa Afrika. Sio lelemama, bwana, jamaa alikimbiza mbaya!. Hapo Diamond Platnumz akamchukua, wakaanza kutikisa pamoja.

Alafu, kama hujaskia “Happy Birthday” au “Sina,” umelala bro. Hizi ngoma zilimkuza zaidi hadi 2017 aliporudi na “Kwa Ngwaru”—ile collabo nyingine na Diamond, na hapo watu walijua huyu jamaa hayuko hapa mchezo. 2018 akashirikiana na Skales kwenye “Fire Waist,” club anthem ya ukweli.

Halafu, 2019 akatupa EP yake ya kwanza Afro Bongo na kuanzisha lebo yake—Konde Music Worldwide. Jamaa hakuishia hapo, akafanya kazi na kina Sheebah, Eddy Kenzo, Phyno, na hatimaye akashusha Afro East 2020. Yani, safari yake ni kama movie, full action na surprises.

Nyimbp Mpya kabisa za Harmonize

TOPWAP.LT